Zuchu – Naringa Lyrics – citiMuzik

Dive into the lyrics of “naringa” from Zuchua unique fusion of Amapiano, African Gospel and Zuchu’s distinctive Baibuda style.

RELATED: Lony Bway – Wewe Hapo Ft Marioo LYRICS

Zuchu – Naringa Lyrics

To sing! Mmmmh, Eeeeh!

Let’s sing, come on, Eeeh

Sioni aibu kwa kila linalonifika

Mana kukosea ni wajibu

Mola ameshaandika

Na sianguki mimi nimechaguliwa

Nnaemtegemea hachoki

Hajawahi kupitiwa

Mnavyotuma-Viniue

Ndo vinanikuza

Vinanipa ujasiri na kuwa

Gado kamili

Ukitaka kunidhuru mie

Upite kwake kwanza

Mungu Wangu Halali

Ana ulinzi mkali

Na ndio maana naringa naringa

Naringa Naringa Naringa

Nalindwa na Mungu

Msinione navimba navimba

Navimb navimba navimba

Nalindwa na Mungu

raise your glass

Cheers to the Lord

Roho Mbaya ubinafsi

Hajaumbiwa nyungunyungu

Wala mtu mwenye maarifa

Kweli mabaya sikosi

Najua Mazuri Yangu

Mtayasema nikifa aaaeh!

Unaniona napambana

Kwa taboo na dhoruba

Nilinde virogo vya

Walimwengu visinifike ng’o

Utadhani wao hawana

Umewapa vikubwa

Ila bado hiki kidogo changu

Kinawatoa Roho

Eeeh na sianguki mimi nimechaguliwa

Nnaemtegemea hachoki

Hajawahi kupitiwa

Mnavyotuma-Viniue

Ndo vinanikuza

Vinanipa ujasiri na kuwa

Gado kamili

Ukitaka kunidhuru mie

Upite kwake kwanza

Mungu Wangu Halali

Ana ulinzi mkali

Na ndio maana naringa naringa

Naringa Naringa Naringa

Nalindwa na Mungu

Msinione navimba navimba

Navimb navimba navimba

Nalindwa na Mungu

DevanCole

DevanCole is a Dailynationtoday U.S. News Reporter based in London. His focus is on U.S. politics and the environment. He has covered climate change extensively, as well as healthcare and crime. DevanCole joined Dailynationtoday in 2021 from the Daily Express and previously worked for Chemist and Druggist and the Jewish Chronicle. He is a graduate of Cambridge University. Languages: English. You can get in touch with me by emailing: devancole@dailynationtoday.com.

Related Articles

Back to top button